}

WAZIRI SIMBACHAWENE AFUNGUA MKUTANO MKUU JESHI LA MAGEREZA.

 Na. Geofrey Jacka - Dodoma


WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi George Simbachawene (Mb), leo September 01, 2021, ametembelea Makao makuu ya Jeshi la Magereza Msalato Jijini Dodoma, na kufungua Mkutano Mkuu wa Maafisa waandazi wa Jeshi hilo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Simbachawene amesema, amefurahishwa na Kasi ya maendeleo inayofanywa na Jeshi la Magereza, hasa katika ununuzi wa vifaa vya kilimo ikiwemo mitambo ya kuvunia na uanzishwaji wa Viwanda mbalimbali.

Waziri Simbachawene (aliyevaa miwani) akipiga makofi Mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda Cha Mikate Msalato.

"Huu ni mkutano mkubwa Sana, wenye lengo la kujadili Mambo ya uendeshaji wa Jeshi la Magereza, kwaiyo nichukue fursa hii kusema kwamba mnafanya kazi nzuri Sana, na Jeshi la Magereza limebadilika Sana, kila sehemu unayotembelea kuna miradi mbalimbali inaendelea, viwanda, nyumba za makazi" aliongeza Simbachawene.

Kabla ya ufunguzi wa mkutano huo Waziri Simbachawene aliweka mawe ya msingi katika Jengo la Kiwanda Cha Mikate Msalato na Tanki la kuhifadhia Maji lenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya Lita laki moja za maji, kwaajili ya kuhudumia Maafisa na Askari wanaoishi maeneo ya Msalato.















No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.