}

CGP - MZEE AZINDUA ZAHANATI GEREZA MSALATO, 'AUPA TANO' UONGOZI.

 Na. Geofrey Jacka - Dodoma.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Meja Jenerali Suleiman Mzee, leo Agost 27, 2021, amezindua Zahanati ya Gereza Msalato, na Kuupongeza uongozi wa Kituo hicho.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mzee amesema kuwa, anawapongeza viongozi wa Gereza hilo kwa Jitihada kubwa walizozifanya, katika kuhakikisha wanakarabati kituo hicho, ili kuweza kutoa huduma bora kwa Jamii inayowazunguuka.


"Niwapongeze sana kwa jitihada mlizozifanya, mwanzoni nilipokuja hapa hali haikuwa nzuri, nikalalamikia hilo na mkanielewa, nafurahi sana leo nimepata nafasi ya kuzindua, mmefanya kazi nzuri, nimeangalia Famasi Madawa yamejaa, hivyo hii inanitia Moyo kuwa hata ujenzi wa Hospitali kubwa tunayojenga Veyula tutafanikiwa" aliongeza CGP. Mzee


Kwaupande wake Mtaalamu wa Maabara wa kituo hicho Stafu Sajini Zuhura amesema kuwa, anamshukuru Jenerali Mzee kwa uzinduzi wa Kituo hicho, huku akimuomba kuwafanikishia Ujenzi wa Hospitali kubwa inayoendelea kujengwa Veyula Jijini Dodoma.


Zahanati hiyo ya Gereza Msalato Jijini Dodoma, imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wanaozunguuka eneo hilo, ambapo huduma za Mama na mtoto pamoja na vipimo vya Maabara zimekuwa zikitolewa kwa ufanisi mkubwa.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.