}

CGP MZEE AWAWEKA MAFUNDI 'KITIMOTO', AHIMIZA USHIRIKIANO.

 Na. Geofrey Jacka - Dodoma


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee leo Septemba 06, 2021, amefanya kikao na Wahandisi pamoja  na Mafundi wa kada mbalimbali wanaofanya kazi makao makuu ya Magereza Jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho Kamishna Mzee amesema kuwa, kila mmoja anatakuwa atimize wajibu wake, huku akisisitiza zaidi ushirikiano baina yao ili kuhakikisha kazi zinaenda vizuri.


"Niwaambie tuu ukweli, kazi mnayofanya ni kubwa, kwaiyo tuendelee kushirikiana, sio Engineer (Mhandisi) wa Saiti hii, anashindwa hata kwenda kwenye Saiti ya mwenzake kushauriana, tukifanya hivyo hatutafika, tunafanya kazi moja hivyo tusitafute sifa ya mtu mmoja mmoja, leo hii akija hapa mtu kwenye ukumbi haitajulikana kipande hiki alijenga fulani na hiki fulani, bali mafundi wote tunaonekana tumehusika" aliongeza CGP MZEE.

Aidha Kamishna Mzee amewataka mafundi kufanya kazi kwa uaminifu na kuepuka ubadhirifu wa vifaa mbalimbali vya ujenzi, kwani kufanya hivyo kunarudisha nyuma jitihada za ujenzi unaoendelea.

Kupitia mkutano huo zimejadiliwa pia changamoto zinazowakabili Mafundi katika utendaji wao kazi wa kila siku, na kuahidiwa kutatuliwa ili kuleta ufanisi katika kazi.


Kwaupande wake Msemaji wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP, Justin Kaziulaya, amewataka Mafundi hao kutokukaa na changamoto za kazi kwa muda mrefu, bali watumie fursa za kuwa karibu na viongozi ili kuzifikisha changamoto hizo ili ziweze kutatuliwa kwa haraka.

Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho,  CGP Mzee, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Jiko na Sehememu ya Chakula, pamoja na Majengo mengine yanayoendelea katika ofisi za Makao makuu ya Magereza Msalato Jijini Dodoma, na kumuagiza Mhandisi Philemon Belela kuhakikisha Jengo la  Sehemu ya Chakula linawekwa Milango leo hii, ili lianze kutumika.

Jenereta kubwa kwaajili ya Umeme wa dharura endapo kutatokea tatizo la kukatika kwa Umeme katika ofisi za Makao makuu ya Magereza, Msalato Jijini Dodoma.






No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.