}

KAMATI YA UKAGUZI WIZARA YA MAMBO YA NDANI 'YATINGA' MAGEREZA.

 Na. Geofrey Jacka - Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Meja Jenerali Suleiman Mzee (kushoto) akielezea Jambo kwa Kamati maalumu ya Ukaguzi kutoka Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi.

KAMATI maalumu ya Ukaguzi kutoka Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, leo Septemba 08, 2021, imefanya Ziara ya Kikazi Makao makuu ya Jeshi la Magereza Msalato Jijini Dodoma.

Kupitia Ziara hiyo Kamishna Jenerali Suleiman Mzee amepata fursa ya kuileza Kamati changamoto na namna alivyoliongoza Jeshi katika safari ya kuhamia Jijini Dodoma na kuanza ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu, kitu kilichoonekana kutowezekana mwanzoni.

"Mara baada tu ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza kule Dar es salaam, sikutaka kuchelewa, haraka sana tukahamia Dodoma, ikumbukwe Rais wa wakati ule Hayati Magufuli alishatoa maelekezo ya Serikali kuhama Dar kuja Dodoma, kwakweli haikuwa rahisi, tulianzia na ofisi za Muda kule Isanga, lakini Muda mfupi tukaanza ujenzi wa hizi Ofisi mnazoziona, na niliposema tunajenga sikueleweka mwanzoni, kwasababu watu walijiuliza tutajengaje?"  alisema Jenerali Mzee.

"Lakini muda mfupi baadae nilianza kueleweka, majengo yakasimama na tukahamia, niwaeleze tuu, tulihamia hapa hata baadhi ya Ofisi zikiwa hazijakamilika, lakini kazi ikaendelea, na nikamuomba Mh. Rais Magufuli aje kuzindua akakubali, na ilipofika Mwezi Februari majengo yakazinduliwa" aliongeza Mzee

Aidha Kamati hiyo iliyojumuisha wajumbe  Watano, ilipata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa ikiwemo Kiwanda cha kuoka Mikate Msalato, Nyumba za Makazi ya Maafisa na Askari, Tanki la kuhifadhia lenye ujazo wa zaidi ya Lita laki moja, Kiwanda cha Samani Msalato, ili kujionea shughuli zinazofanyika, ambapo kwa pamoja wamempongeza Jenerali Mzee kwa jitihada anazoendelea kuzifanya katika kulijenga Jeshi la Magereza.









No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.