}

SERIKALI KUPUNGUZA IDADI YA WAETHIOPIA MAGEREZANI - NAIBU WAZIRI CHILO.

 Na. Mfaume Ally


Serikali iko mbioni kutatua na kupunguza tatizo la idadi kubwa ya raia wa Ethiopia walioko katika Magereza mbalimbali hapa nchini. 

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Hamza Chilo (kushoto), akila chakula ambacho huliwa na Wafungwa na Mahabusu wa Gereza kuu Maweni.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo  ya ndani ya Nchi, Mh, Hamza Chilo alipotembelea Gereza kuu Maweni Jijini Tanga ambapo katika Gereza hilo kuna  jumla ya raia wa Ethiopia 496 idadi ambayo huzidi  Mahabusu na wafungwa raia wa Tanzania, hali inayo pelekea Magereza kuelemewa na mzigo wa kuwahudumia.

''Hili nalichukua naenda kukaa na Kamishna wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Mzee na Mh. Waziri tujadili, kwasababu tumekua tunawahudumia kwa muda mrefu na hawafanyi kazi, na tumeona idadi yao ni wengi kuliko hata wenyeji wa Tanzania waliopo Gerezani, kwahiyo lazima tuchukue hatua madhubuti kuhakikisha tunapunguza idadi hii, kama sio kumaliza kabisa''. Amesema Mh. Chilo.

Aidha Mh. Chilo katika ziara yake hiyo alitembelea mpaka wa horohoro unao unganisha nchi ya Tanzania na Kenya.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.