}

MAAFISA WA MAGEREZA 300 NGAZI DARAJA LA PILI WAHITIMU

 Na. Stephan Ngolongolo - Dar es salaam


Naibu Kamishna wa Jeshi la Magereza, DCP. Jeremiah Katungu, amefunga mafunzo ya uongozi maafisa ngazi daraja la pili, kozi namba 45 katika Chuo cha taaluma ya urekebishaji Ukonga Jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo hayo DCP. Katungu, amewaasa Maafisa hao kwenda kuwa wabunifu katika utendaji wao kazi, ili kuweza kuibua miradi itakayoweza kulisaidia Jeshi katika dhima ya kujitegemea.

"Kwanza kabisa niwapongeze kwa kuweza kumudu Mafunzo mpaka kufikia siku ya leo tunapofunga Mafunzo, lakini nataka Mkawe wabunifu katika utendaji kazi wenu, muende mkabuni miradi itakayowezesha Jeshi kusonga mbele zaidi, lakini mkawe viongozi wa mfano kwa Askari wa chini yenu, mtende haki katika kuchukua maamuzi pindi wanapokosea, msimuonee mtu, lakini pia mkawe Maafisa wenye nidhamu". Amesema DCP. Katungu 

Aidha amewataka kushiriki vyema na kuibua hoja zenye manufaa pindi watakapopata nafasi ya kushiriki katika vikao vya ulinzi na Usalama vya Wilaya watakazo kuwepo.

Jumla ya Maafisa  300 wameweza kuhitimu, huku watatu wakishindwa kutokana na sababu mbalimbali.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.