}

TANZANIA PRISONS YASHUSHA VIFAA VINGINE VITATU, YUPO MMOJA KUTOKA U-20.

Na. Steven Ngolongolo - Dodoma.

Wachezaji waliosajiliwa na Prisons hivi karibuni makao makuu ya Magereza Jijini Dodoma.

Katika kuelekea msimu mpya  wa ligi kuu Tanzania bara 2021/2022 timu ya Tanzania Prisons imeendelea kukiimarisha kikosi chake, kwa kusajili wachezaji wengine watatu watakaotumikia timu hiyo.

Wachezaji waliosajiliwa ni Athanas Mdam kutoka Kariobang Sharks inayoshiriki ligi kuu nchini Kenya  (middlefield), Hassan Peter Msham ambaye alikuwa majeraha mda mrefu(golikipa), huku Ibrahim Abdalah akipandishwa kutoka timu ya vijana wenye umri wa miaka 20 akicheza katika nafasi ya ulinzi.


Akiongea na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa ufundi wa timu ya Tanzania Prisons Kelvin Ferdinand amesema kuwa mpaka sasa Prisons imeshasajili wachezaji saba ambapo watatu ni kutoka timu mbalimbali, na wachezaji wanne  kutoka timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20.

“Tumeshasajili Vyuma Saba mpaka sasa, na tunaendelea kukisuka kikosi chetu, ili msimu ujao kiwe bora na moto wa kuotea mbali, ndio unaona tupo makini Sana katika kipindi hiki, na hatuokoti tu ilimradi wachezaji, tunaangalia wenye uwezo mkubwa wa kusakata gozi”amesema Kelvin."
Kijana aliyepandishwa kutoka Under 20, Ibrahim Abdalah (katikati) akisaini mkataba kuitumikia Taanzania Prisons msimu wa 2021/2022.

Kufuatia usajili huo Kocha wa Tanzania Prisons Salum Mayanga amesema kuwa, yeye sio Kama makocha wengine wanaosajili kwa mbwembwe, bali yeye Mara zote ni mkimya lakini majibu yake yanaonekana uwanjani Ligi inapoanza.

"Mara zote Mimi sio muongeaji, huwa naanza hivi Kama Masihara, lakini majibu yanaonekana uwanjani Ligi ikianza, Sina mbwembwe Kama wenzangu" aliongeza Mayanga.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.