}

JESHI LA MAGEREZA LAAHIDI MAKUBWA MASHINDANO YA MAJESHI.

 Na. Steven Ngolongolo

Mkurugenzi wa Michezo wa Jeshi la Magereza ASP. Francis Taabu, akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Mashindano ya Majeshi.

Jeshi la Magereza limejiandaa vyema na michezo ya majeshi inayotarajia kutimua vumbi Jijini Dodoma hivi karibuni.

Akiongea na na waandishi wa habari  Makao Makuu ya Jeshi Jijini Dodoma  Mkurugenzi wa michezo wa Jeshi la Magereza  Mrakibu Msaidizi wa Magereza Silvester  FrancisTabu maarufu Farao amesema, wamejiandaa vyema kushiriki katika mashindano hayo yatakayoanza tarehe Mapema Agosti 04, 2021.

“kama unavyojua Magereza tuna timu imara zenye uwezo wa kushindana  mashinadano yoyote, mfano tuna timu ya mpira wa pete kwa wanawake, timu ya mpira wa miguu Tanzania Prisons zinafanya vizuri katika ligi za ndani,kwahiyo tumejiandaa kushinda katika kila michezo" aliongeza Farao.

Akizungumzia maandalizi ya Mashindano hayo Farao amesema, wachezaji wamefanya mzoezi ya kutosha kuhakikisha wanachukua vikombe na medali za kutosha katika mashindano hayo.

"Mashindano yaliyopita ya majeshi, tulikuwa mshindi wa tatu kwa ujumla, kwa kupata baadhi vikombe na medali katika timu zetu, hivyo haya ya mwaka huu, wenzetu wa Majeshi mengine watatusamehe tu, kwasababu hatutawaacha Salama" aliongea kwa kutamba Farao.

Mwenyekiti wa timu ya mpira wa miguu ya Jeshi la Magereza (Tanzania Prisons Sc) ACP. Mkwanda Mkwanda.

Awali akizungumzia suala la usajili Mwenyekiti wa Tanzania Prisons, Kamishna msaidizi wa Magereza Hasseid Mkwanda akiongea na waandishi wa habari amesema kuwa wamefanya usajili wa mcheza Allon Kalambo kutoka Dodoma Jiji kujiunga na timu ya mpira wa Miguu ya Jeshi hilo kwa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara 2021/2022.

"Tumemsajili Kalambo kutoka Dodoma Jiji Fc, kwahiyo ni Mali yetu na mtaanza kumuona msimu ujao Ligi itakapoanza, Ni mchezaji mzuri sana, na kwa falsafa ya timu yetu nadhani atakuwa bora zaidi" aliongeza Mkwanda.

Alipoulizwa kuhusu golikipa wa Tanzania Prisons Jeremia Kisubi amesema mchezaji huyo kwa sasa  amemaliza mkataba wake na yupo huru.

"Kisubi amemaliza mkata na sisi hivyo yupo huru, siwezi nikasema amechukuliwa na Timu gani, nitakuwa naingilia mipaka ya timu nyingine, wenyewe wakiamua kumtangaza basi itajulikana, Ila ninachojua yupo huru" alisema Mkwanda.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.