}

MSEMAJI JESHI LA MAGEREZA SACP-KAZIULAYA AIPA SIRI TANZANIA PRISONS KUJIIMARISHA KIUCHUMI..

Na. Geofrey Jacka - Dodoma

Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania SACP. Justine Kaziulaya.

Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania SACP. Justine Kaziulaya, leo Agosti 03, 2021 amesema kuwa, uongozi wa timu ya Tanzania PRISONS unapaswa kushirikiana kwa karibu na Waandishi wa Habari wa Jeshi hilo katika kuitangaza timu hiyo.

Akizungumza ofisini kwake na Meneja wa timu hiyo Prosper Mzeru pamoja na waandishi wa Habari wa Jeshi hilo Kaziulaya amesema, ili kufikia Malengo ni muhimu timu hiyo kutangazwa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje, hali itakayopelekea timu kutambulika zaidi hivyo kuvutia wadhamini wengi zaidi, kuliko kujifungia ambapo kutapelekea kukosa ushawishi kwa Jamii.

"Ni vizuri Sana tukafanya kazi kwa pamoja, lazima waandishi washirikishwe ili kuitangaza zaidi timu, lakini pia lazima Timu Sasa iweze kujijenga kiuchumi, iwe na Miradi ya kuingiza kipato, iwe na majengo yake pamoja hostel, hata hapa Msalato tunajenga Uwanja wa Mpira, nafikiri kutakuwa na sehemu za Biashara kuzunguuka Uwanja, hiyo pia iwe ni sehemu ya mapato ya Timu". Aliongeza Kaziulaya.


Kwaupande wake Meneja wa Timu hiyo Prosper Mzeru amesema kuwa, timu ya Prisons ina falsafa ya peke yake kabisa, hivyo hata usajili wake unazingatia vigezo zaidi, pamoja na kujali vipaji vya vijana wetu kutoka Under 20.

"Tunajitahidi Sana tuwe na mfumo mzuri wa usajili, hasa kutumia zaidi vijana wetu wa under 20, itatupunguzia Sana gharama katika usajili, lakini pia ni kuthamini vipaji vya vijana wetu" Aliongeza Mzeru.

Meneja wa Timu ya Tanzania Prisons Prosper Mzeru (Kulia) akizungumza jambo katika kikao na msemaji wa Magereza SACP. Kaziulaya na Waandishishi wa Habari, Kushoto ni Mkuu wa Kitengo Cha habari Magereza ASP. Juma Kapilima.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuwaajiri wachezaji ambao raia Mzeru amesema, sio jambo baya kwa watakaopenda kuajiriwa basi Jeshi lione namna ya kufanya ili waajiriwe.

Akizungumzia suala la Udhamini wa timu Mzeru amesema, Prisons tayari imeshapata mdhamini mkuu kwa msimu ujao wa 2021/2022 ambaye ni SOKABET, lakini bado Kuna nafasi 04 za udhamini, hivyo kama atajitokeza mdhamini mwingine atapokelewa kwa mikono miwili.


"Unajua Tanzania Prisons ni timu kubwa na kongwe ndani ya Ligi kuu ya Tanzania, katika timu nne longer ni pamoja na Prisons, Kuna Simba, Yanga, Mtibwa na Sisi, na Jeshi la Magereza lina watu wengi wanamichezo, hivyo nitoe pia wito kwa Askari hasa wale ambao tayari Wana taaluma ya ukocha leseni C, waende wakajiendeleze wapate leseni B, itasaidia Sana kunoa vijana ambao watakuja kuisadia Timu yetu". Aliongeza Mzeru.



No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.