}

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE AIFAGILIA MAGEREZA KIWANDA CHA MAZIWA.

 Na. Geofrey Jacka - Morogoro.


Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2021 Luteni Josephine Paul Mwambashi, leo Agosti 10, 2021 ameweka Jiwe la Msingi katika Kiwanda cha kuchakata Maziwa kilichopo Gereza Mtego wa Simba  Mjini Morogoro.

Akizungumza Mara baada ya kukagua Jengo la Kiwanda na baadhi ya mitambo ya uchakataji maziwa Luteni Mwambashi amesema kuwa, ameridhishwa na kazi iliyofanywa na  Magereza, na ametaka uwe mfano wa kupigwa wa namna ya kufanya kazi kizalendo katika kusimamia miradi ya mbalimbali ya Serikali.


"Ndugu zangu, mwenge wa Uhuru umekuja hapa kiwanda cha kuchakata Maziwa kinacho milikiwa na Jeshi la Magereza, tumeliangalia Jengo na baadhi ya nyaraka, kwakweli wamekidhi vigezo, nawapongeza Sana kwa kazi nzuri iliyofanyika hapa, na hii iwe mfano wa namna ya kufanya kazi kizalendo, na kuisimamia miradi mbalimbali" amesema Luteni Mwambashi.

Mkuu wa Gereza Mtego wa Simba SP. AD. Mwazembe (kushoto) akielezea Jambo kuhusu moja ya mtambo wa uchakataji Maziwa uliopo ndani ya Kiwanda hicho.

Awali akisoma maelezo kuhusu Kiwanda hicho, Mkuu wa Gereza Mtego wa Simba SP. Mwazembe amesema kuwa, Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuchakata Lita elfu moja za Maziwa kwa siku, hivyo kupitia mradi wao wa Maziwa Kingolwira utapeleka kiwandani Lita 600 na Lita 400 zitatoka kwa Wananchi wanaozunguuka eneo hilo.
 
"Hiki Kiwanda kitasaidia sana kuinua uchumi wa wanachi wa maeneo haya, kwani kitapokea Lita 400 kutoka kwao, na sisi tunatoka Lita 600, hivyo Sasa thamani ya Maziwa itakuwa imeongezeka na kipato cha Mwananchi mmoja mmoja kitaongezeka piaa", alisema SP. Mwasepe
Msemaji wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP. Justine Kaziulaya (mwenye suti ya bluu) na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza, wakifuatilia zoezi la uzinduzi wa Kiwanda hicho.

Kiwanda hicho kinachopo chini ya  Shirika la uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA), kitaanza kazi hivi karibuni Mara baada ya kumalizika kwa zoezi la ufungaji wa baadhi ya mitambo kiwandani humo.
 
Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika picha ya pamoja na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi Mara baada ya uzinduzi.

Jengo la Kiwanda cha Kuchakata Maziwa linavyo onekana kwa upande wa mbele.




No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.