}

SOKA BET RASMI KUIDHAMINI TANZANIA PRISONS SC.

 Na. Geofrey Jacka - Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Klabu ya Tanzania Prisons Sc, Kamishna Msaidizi wa Magereza Mkwanda Mkwanda (kushoto), akiweka sahihi makubaliano ya udhamini.

Kampuni ya kubashiri ya Sokabet imeingia makubaliano ya udhamini na klabu ya Taanzania Prisons kwa kipindi Cha mwaka Mmoja

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wengine wa Soka bet mwanasheria wa kampuni hiyo Erick amesema, makubaliano hayo yamelenga kuungana na wadau na wapenzi wa soka katika kuchochea, kuinua na kuleta maendeleo ya Mpira wa miguu Tanzania.

"Prison ni timu nzuri na inaleta ushindani sana kwenye Ligi kuu ya Tanzania, hivyo sisi Sokabet tumeona ni vizuri kuweka mkono wetu, ili sasa kuifanya iwe na nguvu zaidi" aliongeza Erick.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Tanzania Prisons, Kamishna Msaidizi wa Magereza Mkwanda  Mkwanda amesema, udhamini huo utasaidia kuongeza Chachu ya kupambania nafasi za juu zaidi katika ligi na kuahidi wadhamini kuwa hawata waangusha.

"Kwaniaba ya afande wangu, mkuu wa Jeshi, Meja Jenerali Suleiman Mzee, ambaye ndiye mlezi wa timu,  nawashukuru Sana Sokabet kwa udhamini huu, utaleta Chachu kubwa kwa timu yetu kufanya vizuri, kama Sasa hivi hatuna mdhamini lakini tunamaliza Ligi katika nafasi nzuri, je, Sasa hivi tumepata mdhamini itakuwaje? Naamini sio tu kumaliza katika nafasi nne za juu, bali hata Ubingwa tunaweza kubeba" aliongeza Mkwanda.
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa timu ya Tanzania Prisons, na Soka bet, walipo kutana kukamilisha makubaliano ya udhamini, Regency Park hotel jijini Dar es salaam.

Udhamini wa Sokabet na Tanzania Prisons utawezesha kukidhi mahitaji ya klabu kwa asilimia 100 kulingana na uchumi na mahitaji ya sasa katika kufikia malengo.



No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.