}

NMB YAMWAGA VIFAA VYA MICHEZO MAGEREZA, MASHINDANO YA MAJESHI.

 Na. Geofrey Jacka - Dodoma.

Meneja Mwandamizi Benki ya NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi, Mkurugenzi wa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza Francis Sylvester Taabu.

Meneja Mwandamizi Benki ya NMB, Ally Ngingite, leo Julai 15, 2021, amekutana na Mkurugenzi wa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi Francis Taabu na kumkabidhi vifaaa vya Michezo, ikiwemo Jezi za Michezo yote ikiwa ni maandalizi ya Mashindano ya Majeshi. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Ngingite amesema, Jeshi la Magereza ni mdau wao mkubwa, hivyo msaada huo wa vifaa ni muendelezo wa ushirikiano na mahusiano mazuri baina ya Benki hiyo na Jeshi la Magereza.

"Kwaujumla vifaa tutanavyotoa kwa Majeshi yote vina thamani ya Shilingi Milioni Tano, hivyo Jeshi la Magereza pia ni miongoni mwa Majeshi hayo, vifaa hivi vitaleta Chachu katika Michezo, hivyo niwatake muendelee na mazoezi na msisite kutujulisha endapo kutakuwa na uhitaji wa vifaa mbalimbali" Aliongeza Ngingite.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi Francis Taabu, maarufu 'Farao' amesema kuwa, Kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Suleiman Mzee, anaishukuru Benki ya NMB  kwa vifaa hivyo, kwani vitasaidia kushiriki Michezo ya Majeshi kwa Kujiamini, na ufanisi mkubwa.

"Hivi vifaa vitatusaidia Sana, mashindano yamekaribia hivyo Sasa focus yetu itakuwa kwenye maandaalizi, hasa mazoezi na sio kuwaza vifaa tena, niwashakuru Sana NMB na niwaahidi kwamba Jeshi la Magereza litaendelea kushirikiana nanyi" aliongeza Farao.


Michezo ya Majeshi inatarajiwa kutimua vumbi kuanzia Agosti 04, 2021 katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma, ambapo maandalizi yake yanatajwa kufikia katika hatua za mwisho.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.