}

CHUO KIKUU CHA SHELISHELI CHAISHUKURU MAGEREZA KUSHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA NELSON MANDELA KIMATAIFA.

 


Chuo kikuu cha Shelisheli kimewashukuru washiriki wote ikiwemo Jeshi la Magereza Tanzania bara, kwa kufanikisha kwa mafanikio makubwa mkutano wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela mwaka huu.

Akitoa shukrani hizo kwa niaba ya Chuo hicho, Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti, Amani na Diplomasia Bibi Diana Benoit amesema kuwa, mkutano huo ulikuwa na Mafanikio makubwa kwani washiriki walipata fursa ya kubadilishana uzoefu, na kueleza mafanikio na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa Majukumu yao hususani katika suala zima la urekebishaji wa Wafungwa katika Magereza za nchi zao.

Aidha katika Shukrani hizo Bibi Benoit ameeleza kuwa wanaendelea kuandaa ripoti ya mkutano huo na baadae itasambazwa kwa nchi washiriki ili kuipitia kabla haijatolewa rasmi.

Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya video Julai 23,  mwaka huu, ambao ulishirikisha nchi za Israel, Mauritius, Shelisheli na Tanzania ambayo iliwakilishwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza SACP. Justine Kaziulaya.

Siku ya Nelson Mandela huadhimishwa kila mwaka Kimataifa ili kukumbuka mchango wa mwasisi huyo wa Taifa la Afrika kusini katika Magereza.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.