}

MAGEREZA YASHIRIKISHA WADAU KUANDAA TAARIFA TAKWIMU ZA UHALIFU.

 Na. Geofrey Jacka - Dodoma 

Mkuu wa kitengo cha Takwimu na Tafiti wa Jeshi la Magereza, Kamishana Msaidizi Mwandamizi Salumu Omary, akifungua kikao cha Uandaaji wa Taarifa ya Wahalifu.

Kitengo cha Takwimu cha Jeshila la Magereza Tanzania Bara leo  Juni 22, 2021 kimezindua uandaaji wa taarifa ya Wahalifu jijini Dodoma, uzinduzi uliofanywa na Mkuu wa Kitengo hicho, Kamishna msaidizi Mwandamizi, SACP Salumu Omary.

Akizungumza katika uzinduzi huo SACP Salumu amesema kuwa, zoezi la uandaaji wa taarifa ni hatua za mwisho kuelekea katika uzinduzi wa kitabu maalumu kitakachobeba Takwimu za Wahalifu waliopo Magerezani nchi nzima, na hii ni mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchakataji na uingizaji taarifa katika Kompyuta (Data entry) ambalo lilianza mapema Mei 11, 2021.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya uandaaji wa Taarifa ya Wahalifu ya Jeshi la Magereza, inayoendelea na kazi hiyo eneo la Nanenane Jijini Dodoma, wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati hiyo SACP Salumu Omary (hayupo pichani) alipokuwa akifanya ufunguzi wa kikao.

Aidha SACP Salumu amesema kuwa, uandaaji wa Takwimu ni zoezi wanalofanya kila mwaka na limekuwa na manufaa makubwa kwa Jeshi na Serikali kwa ujumla, kwakuwa mipango na Sera mbalimbali zinanapangwa kwa kufuata Takwimu.

"Hizi takwimu zitaainisha aina ya uhalifu, umri wa wahalifu, vijana, wazee, hivyo itasaidia kujua ni aina gani ya uhalifu na unafanywa na kundi gani katika hayo niliyoyataja, kwahiyo Takwimu ni muhimu sana, kwakuwa mipango mingi pia inapangwa kulingana na Takwimu, na hii itatusaidia pia hata katika kuishauri Serikali kwenye mambo yanayo lihusu Jeshi letu". Alisema SACP Salumu.

Wadau washirikishwa.

Katika mchakato mzima wa uandaaji wa taarifa hiyo yakitakwimu, baadhi ya wadau kutoka katika taasisi mbalimbali wameshirikishwa akiwemo muwakilishi kutoka ofisi ya Taifa ya Mashtaka nchini, Wakili Beata Alois Kittau, muwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mtakwimu Mwandamizi Rainer Gabriel Kiama, na Mtakwimu kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi CPL Habiba, ili kuifanya taarifa hiyo kuwa na ubora zaidi pindi itakapotoka.

Muwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi Beata Alois Kittau akizungumza na Waandishi wa Habari wa Jeshi la Magereza (Hawapo pichani), alipohudhuria kikao cha uandaaji wa taarifa ya Wahalifu ya Jeshi la Magereza.

Wakili Beata amesema kuwa, Ofisi ya Mashtaka ni mdau mkubwa wa Takwimu kutoka katika Jeshi la Magereza na Polisi, na zimekuwa na msaada mkubwa katika utendaji kazi wao, ambapo amelitaka Jeshi la Magereza kuendele kuandaa taarifa hizi kila Mwaka ili kuwe na Muendelezo wa Takwimu.

"Nawapongeza sana Magereza kwa mchakato huu, umefanyika vizuri sana na sisi kama wadau tumeshiriki kikamilifu, kikubwa sasa huu mchakato ufanyike kila mwaka, ili mtu akihitaji taarifa ya mwaka wowote awe anaipata kwa urahisi zaidi". Amesema Beata.

Kwaupande wake Muwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mtakwimu Mwandamizi Rainer amesema, Ofisi yao ni mdau mkubwa wa Takwimu, hivyo ushiriki wao katika michakato kama hii ya uandaaji wa taarifa umekuwa na tija, kwakuwa Takwimu yoyote ya taasisi yoyote haiwezi kutoka kwa Umma bila ya wao kuipitia na kujiridhisha kama ina usahihi.

"Mchakato wa Magereza katika uandaaji huu wa taarifa umefuata vigezo vyote vinavyohitajika, na ndio maana nipo hapa kuendelea kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri, wito wangu sasa hizi taarifa zitakapo kamili zitunzwe vizuri, kwa matumizi endelevu". Amesema Rainer

Mtakwimu Mwandamizi kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu Rainer Gabriel Kiama (Katikati) akiwa katika kikao cha uandaaji wa Taarifa ya Wahalifu.

Muwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Makao Mkuu CPL Habiba amesema kuwa, hii si mara ya kwanza Jeshi hilo kutoa Muwakilishi kwenda kwenye maandalizi kama haya, ambapo amesema kuwa, kumekuwa na ushirikiano mkubwa baina yao, kwani wataalamu wa Takwimu wa Jeshi la Magereza pia wamekuwa wakishiriki katika maandalizi ya Takwimu za Jeshi la Polisi.

"Hii si mara ya kwanza, sisi Polisi tumekuwa na Machapisho mengi sana, na Magereza ni wadau wetu hivyo tunashirikiana nao sana, na huu mchakato wao wa sasa umeenda vizuri, nawapongeza sana". Amesema Habiba.
CPL Habiba kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya uandaaji wa Taarifa ya Uhalifu SACP Salumu amesema kuwa, mchakato huu utachukua takribani siku tano mpaka kukamilika, ambapo pia amemshukuru Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Meja Jenerali Suleiman Mzee kwa uwezeshaji wake mpaka kufikia hatua hii, kwani kumekuwa na uhitaji wa rasilimali Fedha katika uandaaji mzima wa hii Taarifa.

Mrakibu msaidizi wa Jeshi la Magereza ASP Beatrice Kavenuke, akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya uandaaji wa Taarifa ya Wahalifu ya Mwaka 2020, Jijini Dodoma.
























No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.