}

SIMBA WAFANYA MAZOEZI YA KIVITA, WADAI HAWANA PRESHA NA MCHEZO WA KESHO DHIDI YA YANGA

 Na. Geofrey Jacka.

Ikiwa yamebakia masaa machache kuelekea kwenye mchezo mkubwa unaozikutanisha timu kutoka Kariakoo Jijini Dar es salaam, Simba na Yanga, joto limeendelea kupanda miongini mwa mashabiki wa timu hizi mbili, huku mashabiki na Viongozi wa klabu ya Simba wakijinasibu kwa kusema kuwa hawana presha na mchezo huo.
Saido Ntibazonkiza wa timu ya wanachi  Yanga Sc

Timu zote zimeendelea na mazoezi makali kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa jiji Dar, ikiwa ni muendelezo wa Ligi kuu Tanzania bara VPL, mechi inayotajwa kuwa Kali na ngumu ambapo kila Timu inahitaji alama tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kujihakikishia Ubingwa wa Ligi hiyo.
Makocha wa pande zote mbili wamefanya mazungumzo na waandishi wa Habari kuelekea mchezo huo, ambapo kocha Msaidizi wa Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba, Selemani matola amesema, kushinda Mechi ya kesho ni lazima, na hawana presha na mchezo huo, hivyo watashinda ili kujihakikishia Ubingwa mapema ili waendelee ku fokasi na mashindano mengine.
Matola aliongeza kuwa, wanataka wakatoe burudani katika Mechi ya kesho, kwani ndio aina ya uchezaji waliyoizoea siku zote, kwani timu inayomiliki mpira ndio timu inayokuwa na nafasi kubwa ya kupata matokeo, hivyo amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao, na ameahidi hawata waangusha.

Kocha wa klabu ya Yanga, Nabi amesema kuwa mchezo hautakuwa rahisi kwao, hivyo ameandaa kikosi chake vizuri, na wapo tayari kwa mchezo huo.

Mchezo wa kesho Mei O8, utapigwa saa kumi na moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ni wa pili kuzikutanisha timu hizi ndani ya mwaka huu 2021, wa kwanza ukiwa ni ule wa Mwezi January katika kombe la Mapinduzi uliochezwa visiwani Zanzibar, ambapo mchezo uliisha kwa sare, kitu kilichopelekea kupigwa mikwaju ya Penati na Yanga kuibuka mshindi baada ya kufunga Penati nne na kuibuka bingwa wa Kombe hilo la Mapinduzi.

Timu hizi zinakutana huku Simba akiwa kinara wa ligi hiyo ya VPL, ikiwa na alama 61 ikicheza michezo 25, ikiwa na vipolo Michezo miwili, huku Yanga ikiwa na alama 57 ikiwa imecheza Michezo 27, ikifuatiwa na Azam Fc yenye alama 54 huku ikiwa imekwisha cheza michezo 28
Simba Sc wanaingia katika mchezo huo, huku akili zao zikiwa katika robo fainali ya kombe la klabu bingwa Afrika, ambapo wanakabiliwa na mchezo wa ugenini dhidi ya timu kutoka Afrika kusini Kaizer chiefs, mchezo utakao pigwa Jumamosi Mei 15 katika dimba la FNB stadium, majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika kusini huku ikiwa saa moja usiku kwa saa za hapa Tanzania, na mchezo wa marudiano utapigwa dimba la Mkapa jijini Dar es salaam Mei 22 saa kumi jioni.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.