}

ASKARI WANAFUNZI CHUO CHA MAGEREZA KPF WAFANYA ZIARA MAKAO MAKUU, WAFUNGUKA KUHUSU CGP MZEE

Na. Sgt Steven / Sgt Mfaume - Dodoma

Askari Wanafunzi wa kozi ya Maafisa wateule Daraja la kwanza (RSM) kutoka Chuo Cha Magereza KPF Cha mkoani Morogoro, leo Mei 04, 2021 wametembelea Makao makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dodoma, kwa lengo la kujifunza na kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa katika Jitihada za kuliletea Jeshi hilo Maendeleo.
Published from Blogger Prime Android App
Mrakibu msaidizi wa Magereza Mhandisi Malema akitoa ufafanuzi wa namna mitambo ya kiwanda Cha Samani Msalato itakavyo fanya kazi baada ya ujenzi wake kukamilika.

Mara baada ya kuwasili makao makuu Msaloto Wanafunzi hao pamoja na Walimu wao, walipata fursa ya kutembelea ofisi za vitengo vyote, pamoja na miradi mbalimbali ikiwemo Kiwanda kikubwa Cha Samani Msalato, Ujenzi wa nyumba za maafisa na askari pamoja na miradi mbalimbali ya Gereza Msalato, ambapo wamempongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Meja Jenerali Suleiman Mzee kwa Jitihada anazo endelea kuzifanya katika mageuzi ya Jeshi hilo.
Published from Blogger Prime Android App

Mmoja wa Wanafunzi hao Sajin taji Geofrey amesema kuwa, amefurahi Sana kufika Makao makuu hapo, huku akisema dhamira ya mkuu wa Jeshi katika kuleta maendeleo ni thabiti, kwani aliyoyaona hakutegemea,  hivyo ameahidi kwenda kuwa shuhuda na kuhamasisha Maendeleo kituoni kwake mara baada ya kuhitimu kozi hiyo ya RSM.

Published from Blogger Prime Android App

Ziara hiyo ya Siku mbili iliyo ongozwa na mkuu wa Chuo hicho Kamishna msaidizi wa Magereza Lazaro Nyanga, inatarajiwa kuhitimishwa kesho Mei 05, kwa kupata Mada kutoka ofisi ya Utawala ya Jeshi hilo, Ofisi ya Mafunzo, Sheria, Utumishi, Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza (SHIMA) pamoja na Ofisi inayo husika na Masuala ya Pensheni, Kisha mkuu wa Chuo atafanya Majumuisho ya Ziara hiyo kabla ya kuhitishwa na atakayekuwa Mgeni rasmi, Kisha kurejea Chuoni mkoani Morogoro.
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.