SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU AFRICA (CAF) LAIPONGEZA SIMBA KUNYAKUA UBINGWA WA VPL.
Na; Geofrey Jacka.
Shirikisho la mpira wa Miguu barani Africa (CAF) limeipongeza klabu ya Simba Sc kwa kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Tanzania Mara ya tatu mfululizo.
Pongezi hizo zimetolewa kupitia akaunti yao ya mtandao wa Twitter muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo uliowakutanisha Tanzania Prison na Mabingwa hao Simba Sc uliochezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Simba imetangaza ubingwa ikiwa na michezo sita kibindoni ambayo bado haijachezwa kitu kinachoonesha ubora zaidi wa timu hiyo ukilinganisha na vilabu vingine vinavyoshiriki Ligi hiyo ya Tanzania ikiwamo Timu ya Yanga Sc ambao ni wapinzani wakubwa wa wa Mabingwa hao.
No comments