OKWI BADO ANAIWAZA SIMBA? AMUAHIDI CHAMA KUONANA TENA.
Na; Geofrey Jacka.
Aliyekuwa mchezaji wa Timu ya Simba Emmanuel Okwi, ameippongeza timu hiyo kwakutwaa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram @Emmanuelokwi ameweka picha inayoonesha Mabingwa hao wa #VPL Simba sports Club wakishangilia nakuandika "League Champions For Third Consecutive Time!! Well Deserved @simbasctanzania "
kitu kilichopelekea Mashabiki na baadhi ya wachezaji wa Simba kumuandikia maoni (Comment) wakimshukuru na kumkaribisha Tena katika Timu hiyo.
Mmoja kati ya wachezaji wa klabu ya Imba waliomuandikia Maoni ni Straika Clatos Chama ambaye alimshukuru kwa kuwapongeza na kupelekea Okwi kumjibu kwakumwambia "we shall meet again" kitu kilichotafsiriwa na watu wengi kuwa bado ana mapenzi na Klabu ya Simba na huenda ana ndoto zakurejea Msimbazi katika wakati ujao.
Simba imetangaza ubingwa siku ya Jumapili ya tar 28 mwezi wa sita jijini Mbeya ambapo ilicheza na Tanzania Prison wajelajela Orijino katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine na mchezo kumalizika kwa sare ya bila kufungana hivyo kupelekea Simba kufikisha alama 79 ambazo hazitafikiwa na Timu yoyote iliyopo katika Ligi hiyo.
No comments