}

Kuhusu Notisi ya Siku siku 14 Waliojenga kwenye hifadhi ya Barabara, DC-Nachingwea atoa tamko.

Na.Geofrey Jacka.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mh.Rukia Muwango akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo wa kata za Nachingwea mjini (hawapo pichani) alipokutana nao kwa mazungumzo maalum.
Mkuu wa Walaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mh. Rukia Muwango amewataka wananchi wilayani humo  kutii sheria bila bila shuruti hasa kwenye mambo ya Maendeleo.
Wafanyabiashara wa kata za Nachingwea mjini wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya hivyo Mh. Rukia Muwango(hayupo pichani) walipokutana nae kwa mazungumzo maalum ya Maendeleo.
Akizungumza katika Mkutano na wafanyabiashara ndogondogo wa kata za Nachingwea Mjini, Muwango amesema, umefika muda wa wananchi kushirikiana, kuhabarishana, kuelimishana na kuhamasishana masuala mbalimbali ya maendeleo.


Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa  Mh. Muwango amewataka wafanyabiashara na wananchi kwaujumla kutii agizo la Notisi ya siku kumi na nne zilizotolewa kwa wananchi waliojenga katika hifadhi ya barabara huku akisisitiza kuwa Maendeleo ni gharama hivyo ni lazima wakubali.

" Mara ya kwanza notisi zilitolewa 2012, busara ikatumika, lakini sasa umefika wakati tuwaelimishe wananchi kutii sheria bila Shuruti, wenyewe tumeshuhudia  nyumba za ibada, ofisi za Taasisi za umma na binafsi na hata majengo ya wizara mbalimbali yaliyovunjwa ili kupisha ujenzi wa barabara katika maeneo mengine kote nchini, hivyo wana Nachingwea pia tunapaswa kukubaliana na hali halisi" Alisema Muwango.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.