}

MILIONI MIATISA ZATUMIKA UKARABATI CHUO CHA UALIMU NACHINGWEA.

Na.Geofrey Jacka.
Zaidi ya shilingi milioni mia tisa  900,000,000/=
zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya shughuli ya ukarabati Mkubwa wa Chuo cha Ualimu Nachingwea.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi Rukia Muwango(wapili kutoka kushoto mstari wa mbele) akipewawa maelezo na moja ya wataalamu waliopo eneo La ukarabati wakati wa ziara yake chuoni hapo.
Baada ya kufanya ziara katika Chuo hicho Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mh.Rukia Muwango amesema, anaridhishwa na Ukarabati unaofanywa ambao kwa kasi na ubora wa ukarabati unaendana na thamani ya fedha inayotumika.

 "Kiwango cha ubora na kasi ya ukarabati kwakweli ninaridhishwa nayo sana na inaendana na thamani ya pesa inayotumika, hivyo nichukue fursa hii pia kumshukuru  Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli kwa yote mema anayotufanyia Wananachingwea" amesema Muwango.

Muwango ameongeza kuwa ukarabati huu utaleta hamasa ya ufundishaji na hali ya kujifunza  kwa wakufunzi na wanachuo na hata kupendezesha mazingira, lakini Wanachuo wana wajibu wa kutunza miundombinu hii baada ya kukamilika kwa ukarabati.

Huu ndio ukarabati Mkubwa kuwahi kufanyika tangu chuo hiki kijengwe mwaka 1976 na unasimamiwa na Mhandisi Mshauri wa Serikali.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.