}

MAAJABU KABURI LA MBWA NACHINGWEA.

Na.Geofrey Jacka.
Mzungu Phills aliishi miaka ya 50 katika Wilaya ya Nachingwea akiwa mkulima mkubwa wa zao la Karanga, alimpenda sana mbwa wake ambaye alikuwa msaidizi wake wa ndani, alikuwa akimtuma sokoni, Posta, buchani na mahali kwingineko na alikuwa mlinzi wa makazi yake pia, alikuwa rafiki yake wa karibu na alimthamini saaana.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mh.Rukia Muwango akiwa ameketi kuu ya Kaburi la Mbwa wa mzungu Phills wilayani Nachingwea.
Alipokufa mbwa huyo Mzungu Phills alihudhunika mno, na kuomboleza kifo chake. Alimzika na kumjengea Kaburi maridadi sana la zege.

Kaburi lipo umbali wa mita 500 tu kutoka katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nachingwea upande wa kulia kuelekea airport karibu na Mondrane Mess.

Mwaka jana Desemba 2017, Ndugu wa Phills Kutoka Stepford (Ulaya huko) walifika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea nakutoa taarifa kuwa wamekuja kuona Kaburi la Mbwa wa ndugu yao.

Kwa bahati mbaya watu wenye tamaa ya utajiri wa haraka haraka walilivunja miaka ya hivi karibuni wakifikiri kuna mali ndani ya kaburi hilo, waling'oa kibao kilichoonesha jina la Mbwa lakini hawakupata chochote zaidi ya uharibifu tu.

Nitaendelea kukuletea vivutio viiingi vilivyopo Nachingwea, Karibu Nachingwea kwa utalii wa ndani.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.