CONGO KUZINDUA CHANJO YA EBOLA KUFUATIA VIFO VYA WATU 25.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inajiandaa kuzindua mpango wa chanjo ya Ebola, katika juhudi za kuzuwia kusambaa kwa mripuko wa ugonjwa huo hatari.
Shirika la afya duniani WHO limesema idadi ya watu waliokufa kutokana na mripuko wa sasa ni 25, huku visa vipya vikithibitishwa na waziri wa afya wa nchi hiyo katika maeneo ya kaskazini-magharibi.
Kitisho cha ugonjwa huo ambao awali uliripotiwa katika kijiji cha mbali kisichofikika kwa urahisi, kilishika kasi wiki iliyopita, baada ya kuthibitishwa kwa kisa cha kwanza katika mji wa Mbandaka ulio na wakazi milioni 1.2.
Chanzo-DW

No comments