ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 1.3 ZATUMIKA MIRADI YA MAENDELEO NACHINGWEA-DC MUWANGO
Na.Geofrey Jacka-Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi Mh.Rukia Muwango ameweka bayana gharama ya fedha za miradi ya maendelea inayoendelea kutekelezwa Wilani humo.
Akizungumza wakati wa Ukaguzi wa Miradi hiyo Muwango amesema, yupo kwenye utaratibu wa kawaida aliojiwekea kukagua shughuli za maendeleo wilayani kwake, huku akisisitiza umakini zaidi kuelekea Mapokezi Ya Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kufungua miradi hiyo.
"Unajua Serikali imetumia pesa nyingi 1.3 Bilioni katika miradi hii, sasa siwezi kuacha tuu bila kukagua kujua inaendeleaje, na kama unavyojua Mwenge upo mbioni Kuja hapa Wilayani, lazima nihakikishe hatupati dosari kama Wilaya" alisema Muwango.
Miradi inayoendelea kutekelezwa na iliyokaguliwa na Mh.Muwango ni pamoja na Ujenzi wa shule ya msingi, barabara yenye urefu wa KM 2.7, mradi wa maji, ghala la kuhifadhia mazao na zahanati ambayo kwajumla ina thamani ya Zaidi ya Shilingi bilioni 1.3.
"Tunategemea kupokea mbio za mwenge wa uhuru 2018 mnamo tar 22/6/2018 kutoka wilaya ya Ruangwa na tutaukabidhi tar 23/6/2018 wilaya ya Liwale.

No comments