}

BUNGE LICHUNGUZE ZILIPO SHILINGI TRILIONI 1.5 ZISIZOONEKANA-ZITTO KABWE.

Na.Happy Shirima.
Chama Cha Act wazalendo kimelitaka  Bunge la jamhuri ya muungano ya Tanzania  kuchunguze Ziliko 1.5 Triilion zisizoonekana Matumizi yake kwenye ripoti ya CAG kutokana na majibu  ya Serikali Bungeni kutoridhisha.

Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe  baada ya ufafanuzi uliotolewa na Naibu waziri wa wizara ya fedha Ashantia kijazi kuhusiana na kutoonekana kwa Matumizi ya fedha hizo.

"Tumesoma majibu ya Serikali kuhusu hoja ya Ukaguzi wa shilingi 1.5 trilioni za umma ambazo hazijulikani zilipo kama yalivyosomwa na Naibu Waziri wa Fedha asubuhi hii bungeni. Ni maelezo yale yale aliyoyatoa Katibu Mwenezi Taifa wa CCM, ambayo tayari jana yamejibiwa na Katibu Mwenezi Taifa wa ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu. "Alisema Zitto.

Aidha ameeleza kuwa Taarifa ya Serikali ya leo na Taarifa ya Fedha ya Benki Kuu, wanaotunza Fedha za Serikali hazisomani kabisa. Tutaongea na waandishi kueleza hili kwa undani zaidi. Ijulikane tu kuwa akaunti za Serikali kwenye Taarifa za Fedha za Benki Kuu hazina hizo Fedha Naibu Waziri ametaja.

Amefafanua kuwa   ubadhirifu mkubwa wa Fedha za Umma ndani Serikali ni kubwa, kiasi cha majibu ya Serikali kupewa Kiongozi wa CCM kuyasema, na kwa kuwa kashindwa kukonga nyoyo, sasa imebidi Serikali ije yenyewe kuyasema majibu yale yale yaliyosemwa na CCM.

 Kwa mara ya kwanza Zanzibar ikikusanyiwa zaidi ya TZS bilioni 200 Sawa na 20% ya Bajeti nzima ya Zanzibar, makusanyo yote ya TRA Zanzibar na mara 10 ya makusanyo ya Zanzibar kutoka PAYE za Muungano ambazo ndio pekee hukusanywa na TRA huku Zanzibar ikiwa inakusanyiwa TZS bilioni 21 tu na TRA.

Hata hivyo amemwomba Spika wa Bunge aruhusu Ukaguzi Maalum wa matumizi ya Shilingi 1.5 trilioni kupitia Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, kwani hata haya majibu ya Serikali yanapaswa kuhakikiwa kwanza na CAG kabla ya kusomwa Bungeni, jambo ambalo halikufanyika.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.