}

MAGEREZA WANUSURIKA AJALI YA MOTO LINDI, KITUO CHA REDIO CHATEKETEA.

Na.  Geofrey Jacka-Lindi.

Moto mkubwa umezuka katika jengo moja la ghorofa mbili mkoani Lindi nakusababisha taharuki kwa watu waliokuwamo ndani ya jengo hilo.

Moto huo umeanzia katika kituo cha Redio cha mashujaa FM kilichopo ghorofa ya pili nakutekeza vifaa ambavyo gharama yake bado haijafahamika huku taarifa za awali zikitaja hitilafu ya umeme kuwa ndio chanzo cha moto huo.

Jengo hilo pia ndipo zilipo Ofisi za Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi katika ghorofa ya kwanza ambazo zimenusurika na moto huo uliozimwa na Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Lindi.

Taarifa kamili zitakujia kuhusu hasara waliyopata kituo cha Redio cha mashujaa, pamoja na kufahamu chanzo cha moto huo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.