}

WAWEKEZAJI WAFARANSA WAJIPANGA KUZALISHA TANI LAKI TANO UNGA WA MUHOGO LINDI.

Na.Happy Shirima.
Wawekezaji wa kifaransa kupitia kiwanda chao kilichopo Lindi wanatarajia kuchakata unga wa muhogo takribani tani laki tano kwa mwaka,  ambapo mchakato huo utasaidia kuzalisha ajira kwa watanzania walio wengi.

Akizungumza na waandishi wa  habari katika kutimiza siku ya tatu ya kazi ya ujumbe wa Ufaransa, Waziri wa viwanda, biashara na  uwekezaji, Charles Mwijage amesema kumekua na ugeni mkubwa kutoka mataifa tofauti huku lengo lao likiwa ni kutafuta fursa za uwekezaji na biashara hapa nchini.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tpsf) Reginald Mengi amesema kuwa wawekezaji kutoka mataifa tofauti wamekua wakija nchini kutokana na Tanzania kuwa na utajiri mkubwa sio wa vitu tu bali wa amani na utulivu.

Pia amesema wameweza kuwa na ushirikiano mzuri na Wafaransa kupitia mabalozi wetu na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na wawekezaji hao bila kukata tamaa maana wanauwezo wa kukuza uchumi wao kwa kujituma kwa bidii.

Naye Balozi wa Tanzania nchini ufaransa samweli  shelukindo amesema kuwa wanatekeleza diplomasia ya Uchumi na wanaunga mkono juhudi za Rais katika kuifanya nchi iwe katika uchumi wa viwanda.

Hata hivyo amesema kuwa kwa kushirikiana na Tan trade wanatarajia kukutana na wafanyabiashara wa Tanzania ili kuweza kupeleka bidhaa zao kuuza Ufaransa kwani wanasoko kubwa hasa katika bidhaa za kilimo kama Asali, Korosho, Chai na Kahawa.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.