YANGA YAFUZU HATUA YA MAKUNDI ,MANARA AWATAKA KULIPA MADENI
Yanga imefanikiwa kukata tiketi ya kuingia hatua ya Makundi ya michuano ya CAF kwa kuitoa Waloitta Dicha ya Ethiopia katika hatua ya mtoano.
Yanga leo wakiwa mjini Awassa Ethiopia katika mchezo wa marudiano wamepoteza kwa goli 1-0 lililofungwa na Esheti Mena dakika ya 2 ila wanafanikiwa kufuzu kwa ushindi wa jumla ya agg ya 2-1, hiyo ni baada ya mchezo wa kwanza Yanga kupata ushindi wa magoli 2-0 uwanja wa Taifa.
Baada ya ushindi huo na kufuzu hatua ya makundi kuna kiasi cha pesa Yanga watapokea kutoka shirikisho la soka barani Afrika CAF ambacho kinatajwa kukadiliwa kufikia milioni 600 za kitanzania, afisa habari wa Simba Haji Manara baada ya kusikia hivyo ameandika ujumbe wa utani kwa Yanga kupitia instagram account yake.
No comments