}

WARSHA UTAFITI WA UCHUMI YAMUIBUA MAMA SAMIA SULUHU .

Na.Happy Shirima-Dar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi hapo kesho katika warsha ya utafiti wa uchumi iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti ya Repoa ambapo inalenga kuleta misingi ya uzalishaji wenye tija na ushindani katika mazingira na masoko yenye ushindani.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dkt.Donald Mmari amesema kuwa warsha hiyo itawashirikisha wanazuoni, watafiti, watunga sera, watekelezi na wasimamizi, wahisani, sekta binafsi na Taasisi zisizo za kiserikali.

Amesema kuwa kwa mwaka huu mijadala katika warsha hiyo  itajikita kwenye mabadiliko ya mfumo wa uchumi yanayoendelea nchini.

Aidha amebainisha kuwa katika warsha hiyo wataweza kujadili safari ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi mseto na shindani, ukiongozwa na viwanda pamoja na kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo  mwaka 2025.

Ameongeza kuwa warsha hiyo inalenga kujadili na kupata maoni yatokanayo na tafiti na uzoefu wa nchi nyingine, ili yatuongoze katika kushiriki na kuchangia zaidi kwenye juhudi za kujenga uchumi wa viwanda.

Ifahamike kuwa warsha ya mwaka huu itakuwa ya 23 tangu Taasisi ya Repoa ilipoanza kuandaa warsha kuu kwa kila mwaka.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.