LEO NI KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 TANGU ALIPOUAWA MWANAHARAKATI MARTIN LUTHER KING.
Leo ni kumbukumbu ya miaka 50 tangu kuuawa kwa mwanaharakati maarufu wa haki za watu weusi nchini Marekani, Martin Luther King Jr.
Aliuawa Aprili 4, 1968 mjini Memphis, Tennesses akiwa na umri wa miaka 39 , na tayari alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na umaarufu mkubwa duniani.
Alisaidia maandalizi ya mgomo wa mabasi mjini Montgomery mwaka 1955 baada ya mwanamke mweusi Rosa Park kukataa kumwachia nafasi ya kukaa abiria mweupe kwenye basi la abiria, na kuchukuliwa kama moja ya matukio muhimu zaidi kwenye vuguvugu la kupigania haki za binaadamu nchini humo.
Martin Luther King anakumbukwa kwa hotuba yake maarufu ya "Nina ndoto" aliyoitoa kwenye maandamano ya mjini Washington, mnamo mwezi Machi, mwaka 1963, akitoa mwito wa usawa miongoni mwa watu wa rangi zote.

No comments