}

ASILIMIA 70 YA MAENEO YA KIGAMBONI HAYAJAENDELEZWA-DC MGANDILWA.

Na.Anaseli Stanley Macha.

Imebainika kuwa maeneo mengi katika wilaya  ya Kigamboni hayajaendelezwa jambo lilichangia kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu katika wilaya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari MKuu wa wilaya hiyo Mh.Hashimu Mdalingwa amesema hayo yamebainika baada ya kufanya operesheni ya siku sita iliyokuwa na lengo la kuimarisha ulinzi maeneo ya fukwe.kuwajua wamiliki wa viwanja vilivyokaribu na bahari pamoja na  kuangalia miundombinu iliylpo maeneo hayo kama yamefuata sheria

Mh. Mgandilwa amesema baada ya operesheni hyo wamebaini mambo mbalimbali   ikiwemo asilimia 70 ya maeneo hayo hayajaendelezwa jambo lilolelekea uwepo wa mapori ambayo yamekuwa maficho ya waalifu

Aidha Mh.Mgandilwa ametaja jambo jingine kuwa wamiliki wengi wa maeneo hayo bado wana dhana ya kuwa hawana rksa ya kuendeleza maeneo yao

Amesema halmashauri sasa inadhamira ya kuibadili wilaya hiyo kwa kuwa na mipango miji mizuri hivyo wamiliki na wananchi wa wilayani humo waanze kuendeleza maeneo yao kwani kile kilichotajwa kuwakinawazuia sasa hakipo tena na jukumu lote lipo ndani ya halmashauri.

"Nawakumbusha wananchi wangu KDA imefutwa jukumu lililokuwa linafanya na KDA sasa lipo kwenye halmashauri ya kigamboni hivyo tunawaruhusu wananchi kuendeleza maeneo yao lakini lazima wawe na kibali kutoka halmashauri"alisema Mdalingwa

Mh.Mgandilwa pia amewaagiza watendaji katika halmashauri hiyo kuhakikisha wanatoa kibali kwa mwananchi anaehitaji kwa muda wa siku tano.

Katika hatua nyingine amewataka wote watakaochukua kibali cha kuendeleza eneo lake kuhakikisha ndani ya siku 30 awe ameanza kuendeleza eneo hilo vinginevyo hatua nyingine za kusheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kwa upande wake Afisa mpango mji wa halmashauri ya wilaya ya kigamboni Bi.Nice William amesema wameyalokea maelekezao ya mkuu wa wilaya na watafanya hivyo kuhakikisha suala hilo ya utoaji wa kibali unafanikiwa ndani ya siku tano baada ya mtu kuhitaji kibali.

Aidha amesema wanakutana changamoto nyingi ikiwemo watu kutaka kabali cha ujenzi katika eneo ambalo yeye si mmiliki halali wa eneo hilo.

Kigamboni imetajwa kuwa ni eneo la uwekejazaji lenye mazingira mazuri na maeneo makubwa yenye usalama na mindombinu bora ambayo ni rafiki kwa wawekezaji.

Mwenyekiti wa uwekezaji wa halmashauri ya wilaya ya kigambini na Diwani wa kata ya kigamboni mh.Doto D. Msawa amewawataka wawekezaji kujitokeza na kuwekeza katika wilayani humo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.