}

ZIARA YA KATIBU WA CCM WILAYA YA ILALA YAWAFIKIA WANACHAMA ELFU 78.

Wanachama wa CCM Wilaya ya Ilala wameombwa kuendelea kumuombea mwenyekiti wao na Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Katika juhudi zake za kuwatumikia wananchi licha ya baadhi ya watu kubeza utendaji kazi wake.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Joyce Ibrahim wakati wa ziara ya kutembelea matawi na mashina ya CCM kwenye wilaya hiyo  ikilenga kuangalia uhai wa chama na kuwasisitiza viongozi wa matawi na mashina kufanya mikutano mara kwa mara ili wabaini kero za wananchi na kuzitatua.

Aidha ameongeza kuwa wanahitaji viongozi ambao wanawatumikia wananchi na watahakikisha kuwa heshima ya chama inarudishwa kwa wanachama na sio viongozi kwani wote wanahaki sawa ndani ya chama chao.
Kwa upande wake Mwenyekiti CCM Wilaya ya Ilala  Ubaya Chuma amemtumbua mjumbe wa ccm shina namba 14 tawi la sabasaba kata ya Ukonga kutokana na kutokubaliwa na wanachama pamoja na wananchi walio wengi kutokana na kuwa na utendaji mbovu wa kazi , kauli mbaya na kwa wanachama wenzake pamoja  na kuweka mbele maslahi yake binafsi..

Hayo ameyafanya katika muendelezo wa ziara yao ambapo pia  amewataka viongozi wote wa mashina wanaojilimbikizia vyeo, kupunguza vyeo hivyo ili kuwapa nafasi na wengine..

Kwa upande wake Mjumbe wa halmashauri kuu ya mkoa Mashaka Nyadhi amewataka viongozi wa mashina kuhakikisha wanasimamia utaratibu wa uendeshaji wa chama ikiwemo idadi ya wanachama ndani ya shina, uchaguzi uendeshwe kwa mujibu wa katiba.

Ziara hiyo ambayo ilianza Machi 9 -26 mwaka huu imetembelea  kata 26  na ndani ya Jimbo la ukonga na segerea  nakubakiza kata 10 ambazo zitamaliziwa mwisho wa mwezi huu  na kufanikiwa kutembelea mashina zaidi ya elfu mbili pamoja na wanachama 78 eflu  ambapo ziara hiyo imefanikiwa  kwa asilimia 75

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.