}

TIMU YA TAIFA YA KONGO YATOA SABABU ZA KUFUNGWA NA TAIFA STARS YA TANZANIA.

Wachezaji wanne wamejitoa kutoka timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakipinga matayarisho mabovu kuhusika na mchezo wa kirafiki wa kimataifa likiwa ni tukio la pili kama hilo katika siku za hivi karibuni.

Arthur Masuaku kutoka klabu ya Premier League ya England ya West Ham United, Paul Jose Mpoku wa klabu ya Standard Liege ya Ubelgiji, Jordan Ikoko wa klabu ya Avant Guingamp ya Ufaransa na Gaeil Kakuta wa klabu ya Amiens ya Ufaransa waliondoka kambini Jumatatu kwa sababu ya kurejewa kwa matatizo ya usafiri pamoja na utendaji wakati timu hiyo iliposafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kiraifiki dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania.

Kufuatia hatua hiyo Timu ya Taifa ya Tanzania imeshinda Goli 02-0 dhidi ya Timu ya Congo. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.