}

PADRI WA KANISA KATOLIKI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI.

Padri mmoja wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amekutwa ameuawa baada ya kupigwa risasi masaa machache tu baada ya kuongoza misa katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

Mkuu wa dayosisi ya Goma padri Gonzague Nzabanita amesema padri Etienne Sengiyumva aliuawa jana na wapiganaji wa Mai Mai Nyatura.

Padri Sengiyumva alijumuika kwa chakula cha mchana na waumini wa eneo hilo kabla ya kupatikana amekufa kwa kupigwa risasi kichwani.

Chanzo-DW

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.