}

NDIZI,MIHOGO MTAMA VYATAJWA KUCHANGIA KUPUNGUZA MFUMUKO WA BEI

Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Machi, umepungua hadi kufikia asilimia 3.9 ikilinganishwa na asilimia 4.1 ilivyokuwa Februari, mwaka huu.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni mtama kwa asilimia 7.1, unga wa muhogo asilimia 6.7, maharagwe asilimia 3.9, mihogo mibichi asilimia 16.6 na ndizi asilimia 16.7.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema hali hiyo inamaanisha kwamba kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Machi imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Februari.

“Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, nchini Uganda umepungua hadi asilimia 2.0 Machi, kutoka asilimia 2.1 Februari, mwaka huu huku Kenya ukipungua hadi asilimia 4.18 Machi, kutoka asilimia 4.46, Februari, mwaka huu,” amesema.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.