}

YANGA ,SINGIDA KUVAANA PASAKA KATIKA KOMBE LA SHIRIKISHO

Kikosi cha Yanga kimepangwa kukamilisha hatua ya robo fanali ya michuano ya kombe la shirikisho manmo aprili mosi 2018 katika uwanja wa namfua huko Singida.

Siku kadhaa baada ya kukamilika kwa droo ya upangwaji wa ratiba ya michuano hiyo kukamili leo shirikisho la soka Tanzania limetangaza tarehe za michezo yote ya michuano hiyo ambapo itapigwa kukamilisha hatua hiyo.

Yanga ilipangwa kumenya dhidi ya Singida United ambapo singida wao watakuwa nyumbani kuwakaribisha Yanga

Aidha Hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho 'Azam Sports Federation Cup' inatarajia kuanza kutimua vumbi Ijumaa ya Machi 30 2018 kwa mchezo mmoja kupigwa.

Stand United itakuwa ina kibarua dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wake wa nyumbani, CCM Kambarage, mchezo utakaoanza saa 10 kamili jioni.

Baada ya mchezo huo siku ya Ijumaa, ratiba itaendelea tena Jumamosi ya Machi 31 2018 kwa mechi mbili ambapo Tanzania Prisons itaikaribisha JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya huku mechi ikianza saa 8 kamili mchana.

Siku hiyohiyo Azam FC itakuwa inacheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, mchezo utaanza saa 2 kamili za usiku.

Hatua hiyo ya robo fainali itakamilika Jumapili, April 1 2018 kwa mchezo mmoja kuchezwa Uwanja wa Namfua kati ya walima alizeti, Singida United watakaokuwa nyumbani dhidi ya Yanga.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.