}

TSHISHIMBI AWAPIGA BAO OKWI NA BUSWITA


Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kupitia Bodi ya Ligi, limemtangaza Mchezaji, Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Februari.

Kiungo huyo wa yanga raia wa kongo DRC ametwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kupata alama 12,  akifunga mabao matatu na akitengeneza moja.

Tshishimbi amewazidi wachezaji 
Pius Buswita (Young African) na Emmanuel Okwi (Simba SC) ambao wameingia nao katika tatu bora kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo kwa mwezi huu wa pili.

Tshishimbi ambaye ni mshindi wa tuzo hii, atazawadiwa kitita cha milioni moja sambamba na king'amuzi cha Azam TV.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.