}

TTCL YAKUBALIANA KUUNGANA NA KAMPUNI YA MAWASILIANO YA TIGO.

Na. Happy Shirima-Dar.

Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation,limeingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya simu za mkononi TIGO yatakayowezesha wateja wa taasisi hizo kubadilishana fedha na huduma za fedha mtandao kupitia simu zao za mkononi.

Akizungumza katika hafla ya kutangaza ushirikiano huo,iliyofanyika jijini Dar es salaam Mkuu wa Huduma za TTCL PESA Bw. Moses Alphonce amesema kuwa TTCL PESA kwa  kushirikiana na TIGO PESA imewaletea wananchi suluhisho sahihi la mahitaji yao ya fedha kwa njia ya mtandao.

Aidha amesema kuwa TTCL PESA imeazimia kuwapa wananchi huduma za kiwango cha juu kabisa cha ubora na unafuu wa gharama za kutuma,kupokea na kufanya miamala kwa kutumia simu zao.

"Tumedhamiria kubadili mifumo ya malipo yote ya umma na binafsi,yasifanyike kupitia mtandao ili kuongeza usalama na ufanisi wa shughuli za ki uchumi na kijamii",alisema Alphonce.

Hatua hii ni mwendelezo wa jitihada za shirika la Mawasiliano Tanzania kurejea kwa kishindo katika soko la huduma za mawasiliano nchini Tanzania,hadi sasa TTCL imefanikiwa kufikisha huduma za 4G LTE katika mikoa 16 ya Tanzania bara na visiwa vya Pemba na Unguja.

Hata hivyo TTCL imeendelea kuwa mhimili Mkuu wa mawasiliano nchini Tanzania ikiwa inaongoza kwa kutoa huduma ya Data Kwa taasisi za umma na binafsi sambamba na huduma za simu za mezani na simu za viganjani.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha huduma za kifedha kutoka TIGO Hussein Sayed amesema kuwa ushirikiano wa kampuni hizo mbili utapelekea wateja wa TIGO PESA kuweza kutuma pesa moja Kwa moja katika akaunti ya TTCL kwa gharama ileile.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.