}

TANZANIA IMEPIGA HATUA KWA ASILIMIA 0.34 KATIKA USAWA WA KIPATO-REPOA.

Na. Happy Shirima-Dar

Mkurugenzi mtendaji wa REPOA Dkt. Donald Mmari.
Taasisi inayojishughulisha na tafiti uchumi nchini Repoa Kwa kushirikiana na Shirika la umoja wa mataifa la uchumi wa Afrika wametoa taarifa juu ya hali ya usawa wa kipato kwa nchi za Afrika ambapo umeonesha kuwa tanzania imepiga hatua  katika usawa wa kipato kwa asilimia 0.34.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dkt Dornald Mmari amesema kuwa Tanzania ipo vizuri katika usawa wa kipato Ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika zilizopo kusini mwa bara hilo.

Aidha ameongeza kuwa kutokana na changamoto zinazozikabili sekta za elimu, Afya, na maji ni vyema suala la uwekezaji katika sekta hizo likatiliwa mkazo haswa katika sekta ya afya ili kuweza kupunguza vifo vya kina mama na watoto na upatikanaji wa huduma ya maji Safi na salama.
Mkurugenzi wa ofisi ya Takwimu Dkt. Albina Chuva. 
Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt Albina Chuwa amesema kuwa utashi wa kisiasa unahitajika kwa wanasiasa wa nchi za Afrika pamoja na wananchi kujituma kutafuta kipato cha mahitaji yao ya msingi.
Mtafiti wa REPOA Dkt. Emanuel Mapito. 
Naye  mtafiti wa REPOA Dkt Emmanuel Maliti amesemakuwa licha ya uwepo wa baadhi ya maeneo yenye maendeleo mazuri ikiwemo sekta ya elimu kwenye maeneo ya mjini na vijijini bado kunachangamoto kwenye maeneo mengine ikiwemo upatikanaji wa maji safi.

Aidha ameongeza kuwa changamoto kubwa ipo kwenye utofauti wa kipato na maendeleo makubwa kati ya maskini na tajiri  kwenye maeneo ya mjini na vijijini  hivyo jitihadi nyingi zinahitajika katika sera ambazo zitaendelea kupunguza utofauti wa kipato maeneo ya mijini na vijijini  ili kupambana na changamoto hizo.

Kwa upande mwingine kumekuwa na utofauti wa Vifo ambapo utafiti  umeonyesha kuwa Vifo vinapungua kati ya mjini na vijijini na pia ni tatizo mjini huku vifo vingi vikionekana kuwakumba matajiri kuliko maskini.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.