}

RAIS WA CHINA XI JINPING AMESEMA TAIFA LOLOTE LITAKALOICHOKOZA CHINA LITAPATA ADHABU YAKIHISTORIA.

Rais Xi Jinping wa China amefunga kikao cha mwaka cha bunge la nchi hiyo leo kwa kutoa ahadi ya mwanzo mpya wa kuwa na jeshi lenye nguvu.

Amesema nchi yoyote itakayothubutu kuingilia himaya ya nchi hiyo itakabiliana na adhabu ya kihistoria.

Matamshi hayo ni onyo kali kwa kisiwa cha Taiwan chenye utawala wake, dhidi ya jaribio lolote la kuzidi kujitenga na Jamhuri ya China. Aidha Xi Jinping ameahidi mafanikio zaidi ya kiuchumi na kutoa mwito kwa China kuchukua nafasi yake inayostahili kidunia.

Amesema vitendo vyovyote na mbinu zozote zinazolenga kuiangusha China vitashutumiwa na wananchi wa taifa hilo na kuongeza kuwa historia tayari imedhihirisha kuwa ni ujamaa pekee utakaoinusuru China.

Chanzo-DW

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.