}

Simba SC dhidi ya Njombe mji, Mtibwa Sugar Vs Simba SC sasa imepangiwa tarehe ya kuchezwa.

Na. Anaseli Stanley Macha. 
Michezo miwili iliyokuwa imehairishwa Njombe Mji dhidi ya Simba SC 
pamoja na Mtibwa Sugar Vs Simba SC sasa imepangiwa tarehe ya kuchezwa.

Tarehe 3 April 2018 kikosi cha Simba kitashuka uwanjani kucheza dhidi
ya Njombe Mji katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Kikosi hicho pia kitasafiri mpaka Morogoro kucheza dhidi ya Mtibwa
Sugar katika uwanja wa Jamhuri mkoani humo tarehe 8 April 2018.

Mechi hizo zimepangiwa tarehe hizo baada ya kupewa nafasi ya kujiandaa
na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masy SC

Simba waliomba ratiba hiyo isogezwe mbele ili kupata nafasi ya kufanya
maandalizi dhidi ya mchezo huo, kabla ya safari yao kuelekea Misri. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.