}

CHINA YAIONYA MAREKANI KUWA HAIOGOPI VITA NAKUTISHIA KUPANDISHA USHURU BIDHAA ZA MAREKANI.

China imeionya Marekani kwamba haiogopi vita vya kibiashara, na kutishia kuziongezea bidhaa za Marekani ushuru unaofikia dola bilioni 3, katika kulipiza kisasi hatua za Rais Donald Trump dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China.

Trump amesaini sheria inayoziwekea vizuizi bidhaa zinazotengenezwa China na uwekezaji wa nchi hiyo nchini Marekani, akisema hiyo ni hatua ya kwanza miongoni mwa nyingine zitakazochukuliwa.

Wizara ya biashara ya China imeorodhesha bidhaa za Marekani zitakazoongezewa ushuru kwa hadi asilimia 25, zikiwemo matunda, nyama ya nguruwe na mvinyo, lakini haitaanzisha mara moja ushuru huo, kwa hoja kwamba inaacha wazi mlango kwa ajili ya mazungumzo.

Kwa upande mwingine Waziri wa Biashara wa Marekani Wilbur Ross alisema jana Alhamis kwamba hatua dhidi ya China ambazo zililenga ukiukaji wa hakimiliki, na zilikuwa na dhamira ya kuileta China kwenye meza ya mazungumzo.

Chanzo-DW

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.