}

NACTE WAZUIA VYUO 163 VISIVYO NA SIFA KUDAHILI

Na. Anaseli Stanley Macha. 

Baraza la taifa la Elimu ya ufundi Nacte limezuia vyuo 163 kudahili
wanafunzi katika kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na shahada baada
ya kukutwa na mapungufu mengi ikiwemo ukosefu wa walimu wenye sifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkuu wa
ufuatiliaji na Tathimini wa Nacte Dkt Annastela Sigwejo amesema
wamefanya uhakiki kwa vyo 459 kati hivyo yuo 296 ndivyo vinakidhi
vigezo vya kutoa elimu kwa kiwango kinachotakiwa.

Aidha Dkt Sigwejo amewataka waombaji wa udahili  kuahikisha
wanajiridhisha kwa kuangalia orodha ya vyuo vinavyoruhusiwa kudahili
wakati wanaomba kujiunga na chuo.

Vyuo 459 vimefanyiwa uhahikiki kati ya vyuo 580 vilivyosajiliwa huku
vyuo 296 pekee ndivyo vimepewa ruhusa ya kudahili wa nafunzi kwa ajili
ya kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na shahda  kwa muhula wa
udahili wa machi na aprili mwaka huu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.