}

MADAKTARI BINGWA KUTOKA(MOI) WARIDHISHWA NA CHUMBA CHA UPASUAJI HOSPITALI YA WILAYA NACHINGWEA.

Na.Geofrey Jacka-Lindi.
Madaktari bingwa kutoka taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kupitia kampeni ya kufichua watoto wenye ulemavu wa vichwa vikubwa na Mgongo wazi chini ya mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mh. Rukia Muwango,  wameikagua hospitali ya Wilaya hiyo nakuridhishwa na chumba cha upasuaji.
Wakizungumza kutoka wilayani Nachingwea mkoa wa Lindi madaktari hao wamesema, chumba cha upasuaji kinahitaji maboresho madogo ambayo wamekwisha waelekeza viongozi wa Wilaya, huku wao wakidai kuja na vifaa tiba vyote vinavyohitajika katika matibabu ya vichwa vikubwa na Mgongo wazi.
Kwaupande wake Mh. Muwango amesema wameshapata orodha ya watoto wenye matatizo hayo kutoka Wilaya mbalimbali za mkoa wa Lindi na wanaendelea kuwapokea hadi tarehe 10/04/2018 ambapo ndani ya kipindi cha mwezi wa nne watarudi kwaajili ya upasuaji na Ushauri wa kitabibu,  huku akiwataka wananchi wa mikoa ya kusini kuchangamkia fursa adimu waliyoletewa.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.