}

WAMISRI WANAPIGA KURA LEO HII KATIKA UCHAGUZI WA RAIS.

Wamisri wanapiga kura leo katika uchaguzi wa rais. Rais Abdel-Fattah al-Sissi karibu ana uhakika kamili wa kushinda uchaguzi huo.

Mpinzani pekee wa Al-Sissi katika kinyang’anyiro hicho ni Moussa Mostafa ambaye ni mwanasiasa asiyejulikana sana na ambaye tayari aliunga mkono Al-Sissi kuwania urais kwa muhula wa pili.

Waliokuwa washindani wakuu katika kinyang’anyiro hicho walijiondoa au kuzuiliwa kushiriki. Upinzani umewataka Wamisri kuususia uchaguzi ukiuita kuwa kichekesho. Huku ushindi wa Al-Sissi ukitarajiwa, idadi ndogo ya wapiga kura huenda ikazusha maswali kuhusu kuaminika kwa uchaguzi huo.

Chanzo-DW

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.