}

KOCHA SIMBA AAMINI BOCCO ATAIMALIZA AL MASRY KESHO

Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre, amesema matarajio yake katika mchezo wa kesho dhidi ya Al Masry anatarajia kiwango kizuri kutoka kwa Mshambuliaji, John Bocco.

Kuelekea mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Lechantre anaamini Bocco atakuwa kwenye kiwango bora baada ya kuumia mguu kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Bocco aliumia mguu ikiwa ni dakika ya 58 ya kipindi cha pili, na kupelekea kuondolewa huku nafasi yake ikichukuliwa na Mburundi, Laudit Mavugo.

Kwa mujibu wa Goal.com, Lechantre amempa Bocco nafasi ya kufunga bao moja ambao utapigwa Dimbani Port Said, Misri.

Mechi ya awali iliyochezwa Tanzania, ilimalizika kwa timu zote mbili kwenda sare ya mabao 2-2.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.