}

DC RUKIA MUWANGO WA NACHINGWEA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MIFUPA MUHIMBILI(MOI) .

Na. Geofrey Jacka-Lindi.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mh. Rukia Muwango kwakushirikiana na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), wataendesha kampeni yakufichua watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na Mgongo wazi katika Wilaya yake.

DC-Muwango amesema, kutakuwa na matembezi ya hiyari kuanzia ofisi ya Mamlaka ya mji mdogo Nachingwea mpaka viwanja vya Maulidi Siku ya tarehe 23 machi mwaka huu kuanzia saa tatu kamili asubuhi.

Mh. Muwango amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi  kuunga mkono zoezi hilo ambalo litakwenda sambamba na Upimaji wa Afya bure,  kugawa mahitaji ya Watu wa makundi Maalum kama wazee, watoto, walemavu na kadhalika, Pamoja na kupatiwa Elimu ya Afya. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.