}

YANGA KUIFUATA MAJIMAJI KOMBE LA FA HATUA YA 16


Katika droo iliyopangwa leo jijini Dar es Salaam, mechi zote za hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zitafanyika kati ya Februari 22 na 25.

YANGA SC itasafiri tena hadi mjini Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Maji Maji.

Na mbali na Yanga kwenda Songea, vigogo wengine Azam FC watamenyana na KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam, wakati mkoa wa Shinyanga utahodhi mechi mbili mfululizo, kwanza ni Stand United na Dodoma FC na baadaye Buseresere na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kahama.

Mechi nyingine za hatua hii ni; JKT Tanzania watakuwa wenyeji Ndanda FC Uwanja wa Mbweni, Dar es Salaam, Kiluvya United na Tanzania Prisons Uwanja wa Filbert Bayi, Kibaha, Pwani, Singida United na Polisi Tanzania Uwanja wa Namfua na Njombe Mji dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Saba Saba, Njombe. 

Ikumbukwe, mabingwa watetezi wa michuano hii, Simba walitolewa katika hatua ya 64 Bora tu kwa mikwaju ya penalti na Green Warriors ya Daraja la Pili baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.


Warriors nao safari yao ilihitimishwa kwa matuta pia na Singida United pale pae Chamazi katika hatua iliyopita ya 32 Bora.


Na kihistoria Uwanja wa Maji Maji mjini Songea umekuwa mgumu mno kwa Yanga kushinda na mara nyingi matokeo yao mazuri yamekuwa sare katika mechi za Ligi Kuu – na sasa wanakutana katika mechi ya mtoano. Itakuwa shughuli pevu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.