}

washiriki zaidi ya 50 kutoka Tanzania bara na Visiwani walenga kuwasaidia wahanga wa matatizo ya kikatili


Katika kukabiliana na changamoto  za kijamii ikiwemo ubakaji, migogoro ya familia na ulawiti shirika la utu  mtoto (CDF)  kushirikina na jeshi la polisi kitengo cha Dawati la jinsia wameendesha mafunzo ya ushauri nasihi kwa washiriki zaidi ya 50 kutoka  Tanzania bara na Visiwani yakilenga kuwasaidia  wahanga wa matatizo hayo.

Akizindua mafunzo hayo ya siku 5 yaliyodhaminiwa na shirika la CDF Kamishna wa polisi Mussa Ally Mussa  amesekuwa lengo la mafunzo hayo ni kupambana na Changamoto zinazowakabili kiutendaji kazi pamoja na jeshi la polisi lenyewe. 

Aidha amesema kuwa, licha ya kuwa na changamoto kubwa za kupambana na uhalifu lakini wamekua wakikabiliwa na changamoto za kijamii ndio maana wakaamua kueka mafunzo hayo kwa polisi jamii lengo ni kuwasaidia wahanga wa matatizo hayo.

Amesema kuwa,kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo,katika jamii ambazo zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara ikiwemo kubakwa , migogoro ya familia pamoja na kulawiti, kuna umuhimu wa kila mkoa na wilaya katika jeshi la polisi kuwa na kitengo cha ushauri nasihi ili kuweza kutoa huduma zenye ubora na kuwafikia watu wengi.

Katika hatua nyingine amelipongeza Shirika la utu wa mtoto (CDF) kutokana na kutoa kipaumbele  kwa kulisaidia Jeshi la Polisi katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa kuihamasisha jamii pamoja na kuandaa program maalum za kutoa mafunzo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo, Koshuma Mtengeti amesema wamedhamiria kutoa mafunzo mengine kwa makamanda wote wa polisi katika mikoa yote ya Tanzania ili kuhakikisha wanasapoti kazi zinazofanywa na shirika hilo na kutoa michango yao hali na mali.

Hata hivyo amesema wanataka kufanya mabadiliko ndani ya jamii ili kueka ulinzi kwa watoto pamoja na wanawake kutokana na hali ya ukatili wa kijinsia iliopo katika jamii pamoja na kuahidi kuwa wanataka kuyaboresha madawati ya mkoa wa Mara, Dodoma na Dar es Salam.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.