}

WANANCHI KATA YA MANZESE WAMETAKIWA KUONDOA BIASHARA KWENYE MITARO.

Na. Happy Shirima-Dar.

Wananchi wa mtaa wa Mwembeni kata ya Manzese Manispa ya ubungo jijini Dar es salaam wametakiwa kuondoa biashara zao kwenye mitaro ya maji machafu ili kuruhusu suala la usafi kufanyika vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa serekali ya mtaa wa Mwembeni Bw. Nestory Kobelo amesemakuwa walishawaita wafanyabiashara hao ofisini na kuwataka kuondoa meza zao juu ya mitaro ya maji machafu na wengi wao wamekaidi agizo hilo.

Aidha ameongeza kuwa kwa sasa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara hao ikiwemo kutoa meza zote juu ya mitaro pamoja na kuwapeleka baraza la kata kwa ajili ya kupigwa faini.

Sambamba na hayo amewataka pia wajumbe wa nyumba kumi kuhakikisha kuwa wanapeleka majina na taarifa za wananchi wanaohama na kuhamia maeneo yao ili kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi.

Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanafanya usafi kwenye mazingira yao ikiwemo mitaro ya maji machafu ili kuepukana na milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu na kuzaliana kwa mbu ambao hueneza ugonjwa wa malaria.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.