}

WACHINA WAIPIGIA HESABU MIHOGO, WAZIRI TIZEBA AMEWATAKA WAJE KUWEKEZA.

Na. Happy Shirima-Dar.
Makampuni ya China yanayohitaji muhogo yametakiwa kuja nchini Kwa lengo la kuweza kusajiliwa pamoja na kuelekezwa Kwa wakulima ili wakulima hao kuweza kupanda muhogo wenye kiwango wanachokihitaji.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt Charles Tizeba wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari juu ya makubaliano ya kilimo yaliyopo baina ya Wizara ya kilimo ya Tanzania na Wizara ya kilimo ya China ambapo amesema makubaliano hayo yatapelekea wakuliwa kuweza kupata soko lenye uhakika.

Dkt Charles ameongeza kuwa ili kuweza kufanikisha zoezi hilo wameandaa kikosi kazi kitakachoshugulika na zao la muhogo pekee ili kuhakikisha wanaitumia ipasavyo fursa iliyopo ya kuuza muhogo nchini humo.

Aidha Naibu Waziri wa kilimo Dkt Mary Mwanjelwa anatarajiwa kuhudhuria katika maonyesho ya bidhaa za kilimo yatakayofanyika nchini China mwezi May mwaka huu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.